Fanya Kila Selfi Iwe Safi na Ng’avu

Ikiwa na kamera ya mbele ya MP 20, Camon X inakusaidia kuonyesha maisha yako ya ajabu kwa kina na ubora zaidi. Camon X mpya zaidi pia itakufurahisha kwa flashi zake mbili za selfi unazoweza kubadilisha ung’avu ambazo zinakuwezesha kubadilisha ung’avu kwa ishara ili kufaa zaidi mtindo wako.

Ubora wa Juu Papo Hapo

Kupitia utekelezaji wa visindikaji viwili vya picha, usindikaji picha wa kila selfi unapata uimarishaji mkubwa katika kasi na ufanisi. Ikilinganishwa na Camon X iliyotangulia, kamera hii inaweza kuchambua na kusindika data kwa wakati mmoja ili kuwezesha uimarishajimbalimbali wa picha papo hapo. Aidha, inatumia teknolojia ya hali ya juu ya kusafisha picha ili kuhakikisha kiwango kidogo zaidi cha uchafu katika picha ya mwisho.

Endelea Kumakinika

Camon X inakuwezesha kupiga selfi zenye athari ya bokeh licha ya kuwa na lenzi moja pekee. Unda selfi na picha za makundi za ajabu zenye mandhari ya mbele yaliyong’aa na usuli wenye ukungu wa kisanaa. Kuwa huru kuongezea nakshi na raha kwenye selfi zako kwa kutumia athari ya bokeh.

Picha zinazoweza kushirikiwa

Kamera ya nyuma ya MP 16 ni mbadala bora zaidi ya kamera ya kitaalamu, inayofanya kila picha kung'aa na inayoweza kushirikiwa. Pia inakuja na teknolojia ya hali ya juu ya fokasi ya PD, ambayo inafuatilia na kupiga picha za vitu vinavyotembea kwa usafi, kwa hivyo hakutakuwa na picha zenye ukungu. Kasi ya fokasi ya mandhari yenye giza imeongezwa kwa 100% ikilinganishwa na Camon X, unaweza kurekodi hata matukio yasiyotarajiwa kamwe kwa kasi ya juu.

Ona Picha Kubwa Zaidi

Furahia mtazamo ulionenepeshwa kwenye Camon X iliyo na skrini ya HD ya inchi 6. Mipaka miembamba inazingira skrini ili kuleta mtazamo mkubwa ambao hauwezi kuacha kuutazama, inayofanya skrini ya inchi 6 iliyo kwenye Camon X kuonekana kuwa thabiti kiajabu. Kwa sababu ya skrini kubwa zaidi, chochote unachofanya na Camon X, sasa unaweza kukifanya vyema zaidi na Camon X. Aidha, skrini imeimarishwa kwa 10% ili kufikia ung’avu wa nit 500, linalohakikisha skrini kusomeka hata katika mwangaza wa jua wa moja kwa moja.

Fungua kwa Haraka

Twakuletea Face ID, mfumo unaofungua simu yako kwa kutambua uso wako. Ikiwezeshwa na kamera ya mbele ya MP 20, Face ID inatumia ramani ya kina cha uso wako ili kukutambua papo hapo. Ni rahisi kusanidi na kifaa bado kina kisomaji alama ya kidole upande wake wa nyuma kama chaguo nyingine ya kibayometriki ya kufungua simu yako.

Inatoshea Mkononi Mwako Vyema

Jinsi watumiaji wa leo wa simu maizi wanavyotumia vifaa vyao kwa muda mrefu zaidi kuliko hapo awali, Camon X imeundwa kwa njia ya kustaajabisha ili kuiwezesha kushikwa kwa muda mrefu. Muundo wake wa kipekee unatoshea mkononi mwako ni kama iliundwa kwa ajili yako pekee, kwa hivyo hautataka kuiweka chini. Ikiwa imeundwa kupitia teknolojia ya hali ya juu ya kusindika, simu hii ina mwili wa milimita 5.2 katika sehemu nyembamba zaidi.

Utendakazi wa Haraka na Bila Matatizo

Prosesa ya octa-core imesakinishwa ndani ya kifaa hiki ili kukupa nishati ya utumizi wa haraka. Ikifikia GHz 2.0, prosesa hii ya octa-core ina maboresho ya hali ya juu yanayoweza kuhimili shughuli nyingi kwa pamoja. Ikiwa na RAM ya GB 3, ni haraka na bila matatizo iwe unafanya shughuli nyingi au unacheza michezo.

Inadumu Zaidi na Inachaji Haraka

Ikiwa na betri ya ajabu ya mAh 3750, Camon X inasindika shughuli zako za kila siku kwa njia thabiti zaidi. Hisi uhakika zaidi kucheza michezo, kutazama video, kuvinjari Intaneti au kutazama matangazo ya Facebook. Pia ina teknolojia ya TECNO ya kuchaji kwa haraka kupindukia. Kwa kuchaji dakika 10 pekee, simu yako inakuwezesha kupiga picha 1,000.

Android™ 8.1 Maizi Zaidi, Haraka Zaidi na Yenye Nguvu Zaidi

Camon X ni mojawapo ya simu maizi zinazokuja na Android™8.1 - toleo bora zaidi la Android kufikia sasa. Kando na muundo mpya, pia ina vipengele kadhaa bunifu na rahisi kutumia ili kuimarisha huduma yako tamba. Je, uliwahi kuwa na wasiwasi kwamba rafiki yako akikuomba simu yako huenda akaona picha zako za siri? Kipengele cha kufunga albamu kimeongezwa kwenye Camon X kama ghala la picha za siri ili kuficha picha zako za kibinafsi mbali na wengine.