Rekodi Maelezo ya Kina Zaidi kwa Ung’avu

Ikiwa unatafuta simu ya kushughulikia mahitaji yako yote ya selfi, usihangaike kutafua. Camon X Pro inatumia kamera ya selfi ya MP 24 iliyo na flashi mbili zinazoweza kubadilisha ung’avu, zinazowezesha selfi safi kwa ung’avu. Kupitia teknolojia ya hali ya juu ya TECNO ya kupiga picha, nukta 108 zisizoweza kuonekana zinaangazwa kwenye uso wako ili kung’amua umbo la kipekee la uso wako na kutoa selfi asili zaidi.

Ubora wa Juu Papo Hapo

Kupitia utekelezaji wa visindikaji viwili vya picha, usindikaji picha wa kila selfi unapata uimarishaji mkubwa katika kasi na ufanisi. Ikilinganishwa na simu iliyotangulia, kamera hii inaweza kuchambua na kusindika data kwa wakati mmoja ili kuwezesha uimarishajimbalimbali wa picha papo hapo. Aidha, inatumia teknolojia ya hali ya juu ya kusafisha picha ili kuhakikisha kiwango kidogo zaidi cha uchafu katika picha ya mwisho.

Kukuweka Ukiwa Umemakinika

Camon X Pro inakuwezesha kupiga selfi zenye athari ya bokeh licha ya kuwa na lenzi moja pekee. Unda selfi na picha za makundi za ajabu zenye mandhari ya mbele yaliyong’aa na usuli wenye ukungu wa kisanaa. Kuwa huru kuongezea nakshi na raha kwenye selfi zako kwa kutumia athari ya bokeh.

Picha zinazoweza kushirikiwa

Kamera ya nyuma ya MP 16 ni mbadala bora zaidi ya kamera ya kitaalamu, inayofanya kila picha kun’gaa na inayoweza kushirikiwa. Pia inakuja na teknolojia ya hali ya juu ya fokasi ya PD, ambayo inafuatilia na kupiga picha za vitu vinavyotembea kwa usafi, kwa hivyo hakutakuwa na picha zenye ukungu. Kasi ya fokasi ya mandhari yenye giza imeongezwa kwa 100% ikilinganishwa na Camon X Pro, unaweza kurekodi hata matukio yasiyotarajiwa kamwe kwa kasi ya juu.

Mtazamo Bila Kikomo

Tazama Camon X Pro, ni vigumu kutovutiwa na skrini ya 6.0" inayojitandaza hadi kwenye kingo za fremu ya simu, na kuacha tu mpaka mdogo kando na skrini. Skrini ya Camon X Pro ya 18:9 inakupa huduma bora ya mtazamo. Kupitia muundo ambao karibu usiwe na mipaka yoyote, Camon X Pro si kubwa kuliko simu iliyoitangulia, na hii inaifanya kuwa rahisi zaidi kuishika mkononi.

Fungua kwa Haraka

Twakuletea Face ID, mfumo unaofungua simu yako kwa kutambua uso wako. Ikiwezeshwa na kamera ya mbele ya MP 24, Face ID inatumia ramani ya kina cha uso wako ili kukutambua papo hapo. Ni rahisi kusanidi na kifaa bado kina kisomaji alama ya kidole upande wake wa nyuma kama chaguo nyingine ya kibayometriki ya kufungua simu yako.

Inatoshea Mkononi Mwako Vyema

Jinsi watumiaji wa leo wa simu maizi wanavyoshikilia vifaa vyao kwa muda mrefu zaidi kuliko hapo awali, Camon X Pro imeundwa kwa njia ya kustaajabisha ili uishike. Muundo wake wa kipekee unatoshea mkononi mwako ni kama iliundwa kwa ajili yako pekee, kwa hivyo hautataka kuiweka chini. Ikiwa imeundwa kupitia teknolojia ya hali ya juu ya kusindika, simu hii ina mwili wa mm 5.2 katika sehemu nyembamba zaidi.

Kufanya Shughuli Nyingi Bila Matatizo na Hifadhi Kubwa

Camon X Pro ina hifadhi ya ndani ya GB 64 ya kuifadhi miziki yako yote, filamu zako zote na mengi zaidi. Chipseti ya MT6763 pamoja na RAM ya GB 4 zinaifanya simu hii kuwa na haraka kupindukia kwa ajili ya shughuli zako za kila siku.

Inadumu Zaidi na Kuchaji Haraka

Ikiwa na betri ya ajabu ya mAh 3750, Camon X Pro inasindika shughuli zako za kila siku kwa njia thabiti zaidi. Hisi uhakika zaidi kucheza michezo, kutazama video, kuvinjari Intaneti au kutazama matangazo ya Facebook. Pia ina teknolojia ya TECNO ya kuchaji kwa haraka kupindukia. Kwa kuchaji dakika 10 pekee, simu yako inakuwezesha kupiga hadi picha 1,000.

Android™8.1 Maizi Zaidi, Haraka Zaidi na Yenye Nguvu Zaidi

Camon X Pro ni mojawapo ya simu maizi zinazokuja na Android™8.1 - toleo bora zaidi la Android kufikia sasa. Kando na muundo mpya, pia ina vipengele kadhaa bunifu na rahisi kutumia ili kuimarisha huduma yako tamba. Je, uliwahi kuwa na wasiwasi kwamba rafiki yako akikuomba simu yako huenda akaona picha zako za siri? Kipengele cha kufunga albamu kimeongezwa kwenye Camon X Pro kama ghala la picha za siri ili kuficha picha zako za kibinafsi mbali na wengine.