Skrini Kamili na Raha Tele

Skrini kamili ya 6” iliyo na uwiano mkubwa baina ya skrini na mwili inakupa raha zaidi kwenye mtazamo wako. Inaonyesha ulimwengu wa ajabu kwa usafi na ung’avu ulioimarishwa. Kifaa cha skrini kamili kinatoa huduma ya ajabu unapotiririsha video, kusoma vitabu, na kupiga picha kwenye simu.

"Kamera Ng\’avu" Usiwahi Kosa Kila Nyakati

Maishani kumejaa mambo ya kushangaza. Washa kamera yako, na upige kila selfi yako ukitumia kamera ya mbele ya MP 8, na utumie chujio zilizoundiwa ndani ili kurembesha onyesho la hisia zako. Kisha weka alama maishani mwako kwa kutumia kamera ng’avu ya nyuma ya MP 13. Iwe unajirekodi au unarekodi maisha yako, kile kinachoweza kutendeka mara moja maishani kinabadirishwa kuwa picha ambazo kila wakati ziko pale pamoja na SPARK 2.

Mwangaza Maizi na Upigaji Picha Thabiti

Ikiwa na mfumo wake maizi wa flashi, SPARK 2 inakupa huduma ya ajabu ya kupiga picha. Flashi mseto iliyoimarishwa upya ya 2.0, pamoja na flashi mbili za mbele, flashi ya skrini na flashi ya pete ya nyuma, SPARK 2 itakuwepo, usiku au mchana ikikusaidia kupiga picha thabiti.

Onekana kwenye Picha ukitumia Hali ya Picha ya Uso

Weka kamera ya SLR mfukoni mwako. Kamera inatumia ugunduaji uso wa 3D ambao ni sahihi, na pia athari ya bokeh kwenye picha za uso za kisanaa. Hali ya picha ya uso inaweka ukungu kwenye vitu ambavyo si sehemu ya picha yenyewe unayotaka kupiga.

Apecha ya F/2.0 Inaangaza Tabasamu Yako

Kamera inaingiza mwangaza mwingi zaidi kupitia apecha ya F/2.0 nayo flashi ya nyuma inaangaza katika mwangaza mchache ili kutoa mwangaza laini unapotumia hali ya usiku. SPARK 2 inakuwezesha uwe na picha ng’avu, safi, na zilizochangamka wakati wa usiku na katika hali zenye giza.

Fungua Kwa Kutazama

SPARK 2 inakusanya maeneo 128 ya ugunduaji kwenye uso wako na inaweza kukutambua mara moja. Fungua simu yako kupitia kufungua kwa uso kwa njia salama na haraka. Inasoma uso wako na kutambua wewe ni nani. Muundo huu thabiti unakupa kazi na nguvu, wakati wowote na mahali popote.

Android™ 8.1*yenye Nguvu

Mfumo msingi wa uendeshaji umepandishwa ngazi hadi kwenye Android™ 8.1* mpya kabisa. Kila kipengele cha mfumo huu kimeimarishwa ili kufanya maisha yako kuwa rahisi zaidi na fanisi zaidi. Upunguzaji halijoto kwa hatua moja kunakupa huduma tamba bora zaidi. *Spark 2 ina 1GB RAM inayo endeshwa na Android™ 8.1 (Go edition)