Watch The Video

Fungua KAMERA mpya

CAMON 12 Pro imerudi na Kamera Tatu Bora za Nyuma za AI za 16+2+8MP na matekelezo yake manne ya upigaji murwa. Picha Wazi Murwa / Pembe Pana Sana ya 120° / Upigaji Picha wa Makro Mno wa cm 2 / Athari ya Kimaajabu ya Bokeh, zinakupatia fursa ya kunasa matukio maridadi kwa pembe tofauti. Fungua KAMERA Mpya kupitia CAMON 12 Pro, utaona kuwa ulimwengu uko wazi, uko karibu, na ni mpana na angavu zaidi.

Alama ya Kidole kwenye Skrini ya Kibunifu

CAMON 12 Pro imehamisha kibunifu sensa yake ya alama ya kidole iwe chini ya skrini. Rekodi maelezo yako ya alama ya kidole, kihivi, utaweza kufungua CAMON 12 Pro mara moja unapowasha mwangaza wa simu yako na kusongesha kidole chako kwenye sehemu ya alama ya kidole iliyoko ndani ya onyesho. Ufunguaji wa 360° usiokuwa na matatizo, usanifu mzuri zaidi wa mwingiliano, mwonekano jumuishi zaidi; hatua kuelekea kwenye simujanja bunifu na mahiri zaidi.

Skrini ya Mkato wa Nukta ya AMOLED ya 6.4”, Kuutazama Ulimwengu kwa Uwazi na Upana Zaidi
CAMON 12 Pro inatumia Skrini ya Mkato wa Nukta ya AMOLED ya 6.4” ili kukupatia huduma bora ya utazamaji inayofanana na sinema. Uwiano murwa wa kingo-hadi-kingo wa 91% unaleta mwonekano mpana zaidi. Skrini ya AMOLED inakuonyesha ulimwengu angavu zaidi wenye kina na rangi zaidi.
6.4” Skrini ya Mkato wa Nukta ya AMOLED ya 6.4”
91% Uwiano Murwa wa Kingo-hadi-Kingo wa 91%
100000 : 1 Utofautishaji Madhubuti wa 100000:1
Eye Hali ya Ulinzi wa Macho
Picha Binafsi Iliyo Wazi, Angavu, na Maridadi Zaidi
32MP Picha Binafsi ya Pikseli Murwa ya 32MP
F2.0 Kipenyo Kikubwa cha F2.0
AI Hali ya Urembo ya AI
18 Vipimo 18 vya Uso
3D Urembo wa Uso wa Stereoskopu wa 3D
Video Urembo wa Mwili na Urembo wa Video
Mwingiliano wenye Ucheshi - Kibandiko cha AR na Emoji ya AR
Kibandiko cha AR kinafinika maumbile 220+ ya uso na kinasaidia utambulisho kwa pembe ya 120°. Vipengele vya ujanibishaji na urembezaji wa mwangaza pia vinazingatiwa. Toleo maalum lililobinafsishwa la Klabu ya Kandanda ya Manchester City limejengwa kimaajabu kama tuzo murwa.
Huisha emoji unayopenda kwa taswira halisi za uso na jifurahishe zaidi unapopiga picha au kuchukua video - Emoji ya AR - Njoo ushiriki mwingiliano wa kuvutia na marafiki.
Picha Binafsi Iliyo Wazi, Angavu, na Maridadi Zaidi Ili kuendeleza DNA ya Picha Binafsi Wazi ya mfululizo wa bidhaa za CAMON, CAMON 12 Pro bado inaendelea kuikuza lenzi ya kamera iliyo wazi yenye pikseli nyingi. Kanuni pepe mseto na teknolojia ya nne kwenye moja zinafanya picha iwe angavu na wazi zaidi. Ili kukwepa kikomo cha Skrini ya Mkato wa Nukta, taa mbili za mweko zimefichwa kwenye skrini, ili kupitisha mwangaza kamili hata kwenye mazingira yenye mwangaza kidogo.
Usanifu Maridadi wa C
Pumbazwa na pete murwa; CAMON 12 Pro imesanifu pete ya kuvutia ya C kwenye jalada lake la nyuma ambayo inawakilisha mfululizo wa vifaa vya CAMON. Usanifu unaong'ara unaifanya laini unapogusa na mwonekano wa kuvutia unaifanya ivutie watu.
Fungua Kizazi Kipya cha Kamera
Lenzi kuu ya 16MP inalenga ugunduzi wa mandhari wa AI na HDR ya AI; kwa kujumuisha mandhari anuwai ya upigaji na kufikisha uboreshaji unaolingana wa AI, mtumiaji ataweza kupiga picha za kiasili na kimaridadi zaidi kupitia lenzi hiyo.
Kwenye mazingira ya kawaida, CAMON 12 Pro inafikisha picha yenye uwazi murwa kwa Kamera Tatu Bora za Nyuma za AI zilizo nzuri zaidi. Picha zinazopigwa na CAMON 12 Pro zitavutia na zitakuwa wazi bila kifani.
16+2+8MP Kamera Tatu Bora za AI za 16+2+8MP Picha Wazi MurwaPembe Pana Sana ya 120° Upigaji Picha wa Makro wa cm 2Athari ya Kimaajabu ya Bokeh
Lenzi ya pili inaleta picha za Pembe Pana Sana ya 120° na huduma ya Upigaji Picha wa Makro Mno wa cm 2. Hatukuachi tu uuangalie ulimwengu kwa jumla, bali pia tunanasa urembo mzuri zaidi unaokuzunguka.
Athari ya kimaajabu ya Bokeh inaangazia picha kuu ya uso na inatia ukungu kwenye usuli, na kuifanya picha ya uso ionekane vizuri kabisa.
Grafiti ya AR, Turubali Lako la Kuchorea
Wakati huu, huisha ubunifu wako bila kusita! Haushinikizwi tena na mazingira. Unapopata wazo la kibunifu, unaweza kulichora papo hapo kwa kutumia brashi na rangi anuwai na kisha kushiriki michoro na marafiki. Kwenye nafasi ya AR, kuna uwezekano usiokuwa na kikomo unaokusubiri uvinjari.
Kielelezo kamili cha kutengeneza maumbile.
Smartphone ya kwanza sokoni yenye AI ya uundaji kulingana na maumbo tofauti ya mwili. Kazi ya kutengeneza mwili husaidia kuboresha sura yako ya mwili, ikiwa ni pamoja na matiti, hip, kiuno, bega, kichwa au mwili. Ikiwa na mifumo mitatu iliyokwisha setiwa tayari ya athari asilia za uzuri wa mwili, marekebisho ya "Visual UI" pamoja na hakikisho la mara moja tu.
ROM ya 64GB + RAM ya 6GB, Kisindikaji cha Misingi Minane, Kuchaji kwa upesi, Utekelezaji Uliowiana na Wenye Nguvu Zaidi
Kwakua ina ROM Kubwa ya 64GB, mtumiaji ana nafasi zaidi ya kuhifadhi picha, muziki, video, na faili. Usafishaji faili mara kwa mara bila wasiwasi ili kupata hifadhi zaidi. RAM kubwa ya 6GB inaufanya uendeshaji wa mfumo uwe na upesi na mzuri zaidi. Watumiaji wanaweza kufanya shughuli anuwai kwa mara moja na pia kucheza michezo bila matatizo. Pamoja na shughuli iliyoongezwa karibuni ya Kuchaji kwa upesi, ufikishaji wa nishati ulio rahisi na wenye upesi zaidi, bila kujali kuhusu kukosa mwingiliano na ulimwengu.
64GBROM Kubwa ya 64GB
6GBRAM Kubwa ya 6GB
Octa-CoreKisindikaji cha Misingi Minane
Kasi ya Uanzishaji wa Programu Imeongezwa Kwa 50%
Mtiririko wa Michezo Umekuzwa Kwa25%
Kuchaji kwa upesi
Kitufe cha Kisaidizi cha Google kinakuruhusu
Kitufe cha Kisaidizi cha Google kinakuruhusu uunganishe kwa kisaidizi cha sauti cha Google kwa mbofyo mmoja na kinakusaidia usulihishe matatizo kwa busara zaidi. Shughuli za kuburudisha na janja zaidi zinastahiki kusubiriwa!
Toleo jipya kabisa la Android™ 9 Pie & HiOS 5.5
Inakuja na toleo la hivi karibuni la mfumo endeshi na kiolesura cha mtumiaji,, CAMON 12 Pro inakuletea huduma ya mtumiaji iliyo mpya kabisa. Mfumo ulioboreshwa hivi karibuni unafanya kazi kama mshiriki mwerevu kwakua hauleti tu hali zenye ufanisi za kikazi, bali pia unaleta shughuli anuwai za kuburudisha. Kitufe cha Kisaidizi cha Google kinakuruhusu uunganishe kwa kisaidizi cha sauti cha Google kwa mbofyo mmoja na kinakusaidia usulihishe matatizo kwa busara zaidi. Shughuli za kuburudisha na janja zaidi zinastahiki kusubiriwa!