CPU Kuu Inaendesha Shughuli bila Wasiwasi

Ikijivunia kisindikaji cha hali ya juu cha deca-core chenye kasi ya 2.0 GHz, Phantom 6 Plus ina utendakazi wa hali ya juu zaidi katika kila shughuli unayofanya. Ina utendakazi bora zaidi kwa 70% huku ikitumia nishati chache zaidi kwa 30% kuliko matoleo ya hapo awali, jambao linalofanya iwe raha kucheza michezo inayohitaji rasilimali nyingi, kutiririsha video za 4K na kupakua kwa kasi ya 300Mbps kwenye mtandao wa LTE CAT6 kwenye simu hii.

Mtiririko Usiolingana na Mwingine

Ni raha kukaa ukijumuika na marafiki wako wote huku ukicheza micheza au kutirrisha video. Ikiwa na GB 4 za RAM ya DDR3, unaweza kuendesha programu 32 kule nyuma bila kutatizika. Unaweza kutegemea kikamilifu GB 64 za ROM ili kuhifadhi hadi nyimbo 12,000 za umbizo la mp3 au angalau filamu 25 za HD. Kwa usemi tu, inaweza kuhifadhi kila kitu unachopenda.

Mwili Mzima wa Chuma Unaonyesha Uangalifu na Nguvu

Ikiwa mwili 98.1% umeundwa kwa chuma, Phantom 6 Plus imepitia michakato 32 na kuundwa kwa mkono kwa dakika 2,880 ili iwe na mwonekano wa ajabu na nguvu iliyojaribiwa. Ili kutengeneza mwili mmoja, betri isiyo weza kutolewa imeundiwa ndani ya simu ambapo sehemu zote zilizounganishwa zimefungwa kwa skrubu za kitaalamu. Teknolojia thabiti ya kuumba ya nano inatumiwa kuimarisha zaidi nguvu ya mwili mmoja wa simu. Kifuniko cha mbele kimetengenezwa kwa chuma mseto cha aluminiamu na magnesiamu na skrini imetengenezwa kwa kioo cha Corning Gorilla Glass 3 ili kukamilisha mwili mmoja wa chuma, kioo ambacho kinajulikana kwa maisha marefu.

Kifuniko cha Kudumu cha Lenzi cha Kioo cha Yakuti

Kioo cha yakuti cha 9H kimewekwa katika muundo wa aluminiamu ili kupa lenzi ulinzi thabiti, na kuonda wasiwasi zozote ulizo nazo. Anzisha kamera kwa urahisi na uanze kutengeneza picha popote upendapo.

Kamera ya Nyuma ya MP 21 Inarekodi Matukio kwa Usafi

Kamera ya nyuma ya MP 21 ni mbadala bora la kamera ya kitaalmu, inayopiga picha zinazostahili kutuzwa tuzo hata katika mwangaza mchache. Inaendanisha na kihisio cha picha cha Sony IMX230 na flashi ya mwangaza halisi ili kupata uwezo huo wa kupiga picha wa hali ya juu zaidi. Pamoja na teknolojia ya kupiga bicha za ubora wa juu, unaweza kutengeneza picha za ajabu za usafi wa MP 80 kwa urahisi. Ina uwezo wa PDAF, inaweka fokasi kwa sekunde 0.1 ili kuweka kamera tayari kupiga picha. Ikiwa na uvutaji wa kidigitali wa 4X, inakuwezesha kurekodi matukio yote maridadi yaliyo mbali au karibu.

Usalama wa Biashara kupitia Idhini ya Kibayometriki

Kihisio cha alama ya kidole kinakuwezesha kuunda nenosiri lako pekee na kufungua simu yako kwa sekunde 0.3. Anzisha skana ya jicho ili kuunda nenosiri la pili. Skani alama ya kidole na kisha jicho lako ili kufungua simu yako kwa usalama. Pia ni unaweza kuweka manenosiri kwenye failia zilizo na taarifa nyeti. Trustlook, proframu ya kuua virusi tayari imesakinishwa kwenye Phantom 6 Plus kwa hivyo unaweza kutumia programu hii ya USD 9.99 bila malipo.

4050mAh, Chaji ya Haraka Upesi ya Type-C

Ukiwa na teknolojia ya hali ya juu ya kuchaji haraka upesi, unaweza kupata dakika 240 za kutumia unapochaji kwa dakika 10 tu hata wakati betri imeisha kabisa. Uwezo wa kuchaji kwa upande wowote wa USB Type-C kunarahisisha kabisa mchakato wa kuchaji. Shika upande wowote wa kebo ya USB ili kuchaji na uendelee kuunganishwa na ulimwengu.

Vikorokoro Vinavyolingana ndani ya Boksi ya Zawadi

Vikiwa vimeundwa pamoja na simu, vikorokoro hivi vinaimarisha maisha yako maizi. Boksi ya zawadi inajumuisha Iapodi za Boom NB01, Adapta ya Type-C, Zana ya Kutoa SIM, Vazi la Ngozi lenye Dirisha na Kilindaji Skrini Thabiti. Jizamishe ndani ya bass nzito na athari ya tamasha unayoletwa na iapodi. Hisi uhakika wa kushika simu iliyolindwa vyema kwenye mkono wako.

Kiini Thabiti Kinaendesha Ulimwengu Mchangamfu

Katika kiini cha Phantom 6 Plus kuna kisindikaji cha deca-core cha sekeumu tatu cha kasi ya 2.0 GHz chenye muundo wa A72. Imeundwa kwa ubunifu wa 20nm sawia na ule wa Samsung S6. Unaweza kuendsha michezo ya hali ya juu au kucheza video za 4K kwenye kifaa hiki na ufurahie kikamilifu burudani ya kina.

CPU Kuu Inayokusudiwa Huduma Maizi Zaidi

CPU ya Helio x20 inafikia takriban alama 82,000 hadi 85,000 katika kipimo cha utendakazi cha Antutu na kuibuka mshindi katika vipimo vya utendakazi wa single-core na multi-core vya GeekBench, na kukupa utendakazi wa mfumo unaoongoza katika sekta na huduma maizi kabisa isiyolingana na nyingine.

Hakuna Kuchelewa, Raha Nyingi

Simu inaendanisha sambamba na kasi ya vidole vyako unapotelezesha kwenye skrini kwa 50ms na kuskani Facebook kwa 55ms. Inaelewa maagizo ya vidole vyako na kutekeleza mara moja ili upate huduma maizi zaidi.

Utendakazi Bora/Usawa wa Nishati

CPU imeundwa kwa muundo wa sehemu tatu ili kuruhusu shughuli tofauti, na kuamilisha sehemu ya CPU au yote kama inavyohitajika na shughuli. Inatumia nishati chache zaidi kwa 26.3% katika kuskani kurasa za wavuti, chache zaidi kwa 35% katika kurekodi video, chache zaidi kwa 38.3% katika kutelezesha ikoni na chache zaidi kwa 38.8% katika kupiga picha. Kwa ujumla, inatumia nishati chache zaidi kwa 30% kuliko simu maizi ya hali ya juu ya hapo awali na inaleta usawa katika ya utendakazi wa ajabu na utumiaji nishati.

Chochote Unachohitaji katika Kifaa Kimoja

Utendakazi wa CPU unaimarishwa na RAM ya GB 4, jambo linalowezesha kuendesha programu 32 kulw nyuma kwa pamoja bila matatizo. Hautakosa chochote muhimu na cha kuvutia. Phantom 6 Plus inaleta chochote unachohitaji pamoja kwa raha isiyo na kifani.

Kamera ya HD ya MP 21

Ikiwa na apecha ya F/2.0, kamera ya nyuma ya MP 21 inaruhusu mwangaza zaidi kuingia katika jukwa la picha, na kupiga picha safi hata katika hali za mwangaza duni. Ikiwa na uwezo wa 0.1PDAF, inarekodi kila tabasamu yako na kila tukio la safari yako. Hata unaweza kucheza video za 4K au kutazama picha kwa kasi ya 30fps bila matatizo. Nenda na Phantom 6 Plus yako kwenye upigaji picha wa kitaalamu.

Pikseli Thabiti, Safi katika Kila Kipengee

Ikiwa unahitaji makuu katika vipengee, utastaajabishwa na picha safi ahjabu za hadi MP 80 zinazotengenezwa na Phantom 6 Plus. Inaunganisha picha kadhaa za kila tukio ili kutengeneza picha moja yenye usafai wa kuridhisha. Kwa usemi tu, kila kipengee kinaonekana ili kukukumbusha kuhusu matukio ya furaha.

Uvutaji Mkuu, Rekodi Karibu na Mbali

Kifaa hiki kina uvutaji mkuu, unaoruhusu athari ya uvutaji kidijitali wa 4X. Unaweza kupiga picha ya jengo nzima au uvute ndani ili kupiga picha ya sehemu ya jengo hilo kwa usafi thabiti.

Hali Mpya ya Panorama

Anzisha hali ya panorama na usongeze kifaa ili kupiga picha ya kila kitu unachotaka. NI rahisi zaidi kuamilidha utendaji huu na kudhibiti mchakato ili kuwa na matokeo bora.

Hali Mpya ya Usiku

Usiwe na wasiwasi ikiwa jambo lolote muhimu linatendeka usiku. Hali mpya ya usiku inasafisha na kuimarisha ubora wa picha ili kupata picha halisia. Hautakosa kumbukumbu nzuri wakati wowote.

Flashi ya Mwangaza Halisi, Picha Halisia

Ukijua kwamba matukio mazuri hayasubiri, Phantom 6 Plus imewekwa flashi ya mwangaza halisi, inayoangaza mwangaza sawia na mwangaza asilia ili kuoata athari ya ulimwengu halisi. Unaweza tarajia kupiga picha maridadi wakati katika mwangaza mchache.

Selfi ya Pembe Pana ya 85°

Flashi ya mbele inaangaza mwangaza laini kwa usawa na kuwa fanisi katika kusawazisha mwangaza. Inasaidia kamera ya mbele ya MP 8 katika kupiga selfi ng’aavu na maridadi zaidi. Tumia kikamilifu kamera ya pembe pana ya 85° na marafiki wengi zaidi washiriki katika kumbukumbu sawia.