Mwonekano Mkubwa, Ulimwengu Mpana

Ikiwa na onyesho la skrini mguso ya MUONEKANO KAMILI wa inchi 5.5, TECNO POP 2 Power hukuonyesha muonekano mkubwa, ulimwengu mpana. Utajihisi kuzama ndani ya kilicho kwenye skrini na kuwa na hali ya utumiaji wa sinema inayovutia.

4000mAh, Kuwa Tayari kwa Muda Mrefu

Ikiwa na betri kubwa ya 4000mAh, POP 2 Power inaweza kudumu hadi matumizi mazito ya siku nzima kwa urahisi. Ungependa kusikiliza muziki? Ungependa kucheza michezo? Ungependa kutazama Video? Hamna tatizo. Hamna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu betri yako kuisha nishati sasa hivi.

Picha ya Kujipiga Inayovutia

Kujipiga picha katika mazingira yenye mwangaza kidogo kumewezeshwa kwa kamera ya mbele ya 8MP yenye mweko. Inakuwa rahisi zaidi kujipiga picha zinazovutia kwa POP 2 Power.

Hifadhi Zaidi

Kumbukumbu ya GB 16 iliyo kwenye kifaa inakupa nafasi zaidi ya kuhifadhi unachokipenda, kama vile filamu, miziki unayopenda n.k. 1GB RAM inakupa hali ya kuridhisha ya simu.

Fungua simu yako kwa Kuitazama tu

Tumia uso kama nywila, fungua kifaa chako kwa kukitazama mara moja tu. Furahia bila bughudha kipengele hichi cha kufungua simu kwa uso mahali popote.

Fungua Simu Yako Kwa Mguso

Rahisisha ufikiaji wa simu ya mkononi kwa usalama unaoweza kuuamini. Kitambuzi cha alama ya kidole kilichojumuishwa ndani hulinda simu yako ili wewe tu ndiye unayeweza kuifungua Kwa mguso mmoja.

Urembeshaji wa AI

POP 2 Power imewekwa madoido ya urembeshaji wa AI, yanayoweza kulainisha ngozi, kuifanya ionekane yenye mvuto sana na macho yakiwa maang`avu. Urembeshaji wa AI unaweza kurekodi tabia zako za urembo na kuunda mienendo yako binafsi ya urembo uliobadilishwa kukufaa.

HiOS 3.3

HiOS 3.3 inatoa maudhui zaidi na ina mawasiliano rahisi. Unaweza kushughulikia faili zako taka haraka zaidi na kudhibiti data vyema zaidi. HiOS 3.3 hii mpya inanuia kukupa hali ya utumiaji rahisi na yenye ufanisi zaidi.