Watch the video

Skrini ya Mkato wa Nukta ya 6.52", Kubwa Kabisa

Wakati huu, SPARK 4 inachukua hatua isiyotarajiwa ya kutumia Skrini ya Mkato wa Nukta ya 6.52", ambayo inakupatia uzoefu halisi mkuu wa mwonekano kamili. Kupitia mwonekano wa juu na uwiano murwa wa skrini wa 90%, ulimwengu unaovinjari kupitia SPARK 4 utakuwa mpana na maridadi zaidi.

Kamera Tatu za Nyuma za 13MP, Kamera Angavu ya AI, Kuwa nyota Ang'avu

Ikiwa na Kamera Tatu za Nyuma za 13MP na Kamera ya Mbele ya 8MP, SPARK 4 inafanya vizuri kwenye upigaji picha nzuri, athari ya bokeh na hali ya picha ya uso ya AI. Picha na picha binafsi zinazopigwa na SPARK 4 zitakuwa maridadi na za kuvutia zaidi kwenye muktadha wowote. Kanuni pepe iliyosombezwa upya ya "Kamera ya 5.0" inaleta AI HDR, Utambuzi wa Mandhari ya AI na shughuli murwa zaidi za upigaji picha. Hata kwenye mandhari ya taa ya nyuma, SPARK 4 bado inaweza kuwa angavu na wazi zaidi, kwa kuepuka ufichuzi kupita kiasi wa sehemu za mwangaza na kuonyesha kwa uwazi maelezo ya giza. Kwa kushikamana na asili ya Kamera Angavu ya AI, SPARK 4 inaukwepa upungufu huu na inaficha tochi zake kwenye skrini ya mkato wa nukta. Bila kuogopa kama ni usiku, daima utakuwa nyota ang'avu kwenye picha.

Yenye Mantiki, Yenye Mtiririko na Nguvu, Zaidi Kuliko Matarajio Yako

ROM ya 32GB inampatia mtumiaji nafasi zaidi ya kuhifadhi picha, muziki, video, na mafaili. RAM ya 2GB inamaanisha uzoefu wa mtumiaji wenye upesi na mtiririko zaidi kwenye mfumo wetu. Kisindikaji cha Misingi Minne cha 2.0GHz kinakuja na utumiaji nishati kidogo na kasi kubwa zaidi ya uendeshaji. Wakati huu, kufanya shughuli nyingi kwa wakati mmoja kutakuwa rahisi na kwepesi zaidi. Betri kubwa ya 4000mAh inampatia mtumiaji muda zaidi wa kuingiliana na ulimwengu.

Mtandao wa 4G, Muunganisho wa Upesi

Kupitia 4G, daima utakuwa wa kwanza kujua mienendo na habari za hivi karibuni kwenye zama hizi zinazoendelea kwa upesi. Kwa kutumia mtandao wa 4G kwenye SPARK 4, punguza muda wa kusubiri kwa ufanisi unapokuwa unavinjari mitandao ya kijamii au unatazama video, na upate burudani zaidi bila kususbiri.

Toleo la Hivi Karibu la Android™ 9 Pie & HiOS 5.5

Kwa kuboresha toleo la hivi karibuni la mfumo endeshi na kiolesura cha mtumiaji, mabadiliko murwa na yenye kuburudisha zaidi yanakusubiri uyavinjari. Wakati huu, huhitaji tena vipodozi, Hali ya Urembo ya Gumzo la Video ya AI itakufanya ung'are kwenye gumzo la video, ambayo inaongeza furaha zaidi unapozungumza na marafiki. Kwa uboreshaji uliobinafsishwa kwa kina zaidi wa Hali ya Mchezo, utapitia uzoefu wa kuvutia wa michezo. Unda nafasi tupu, ukuzaji michezo, uharakishaji mtandao, uboreshaji wa taarifa na shughuli mpya zaidi zinachangia kuleta uzoefu wa mtumiaji ulio tumbukizi zaidi na wenye upesi zaidi. Shughuli za kimsingi pia zina masasisho muhimu. OTG pia ipo. SPARK 4, daima inajaribu sana kuwapatia watumiaji wetu maisha janja mazuri zaidi.

Kufungua kwa Uso 2.0 , Ufunguaji Salama Zaidi

Fungua simu yako kwa upesi kupitia "uchanganuzi wa uso". Rekodi maelezo yako ya uso, SPARK 4 itajifunza na itatambua uso wako unapowasha mwangaza wa simu yako na kuifungua. Kupitia “Utambuzi wa Macho Yaliyofumbwa” iliyoongezwa upya kwenye toleo la 2.0, huna wasiwasi wa kufungua simu yako unapokuwa unalala au unapokuwa umefumba macho.

Usanifu wa Upinde wenye Rangi, Mtindo Tosha

Usanifu mzima hauna madoido, lakini una rangi shupavu. SPARK 4 inasanifu majalada 4 ya nyuma ya upinde wenye rangi - Zambarau Falme/Buluu Likizo/Kijivu Ukungu/Chungwa Changamfu -. Machaguo ya rangi yanayovuta makini yatakufanya uwe na kifaa kisichokuwa na kifani.