Picha Angavu na Wazi

Kanuni pepe iliyo mpya kabisa ya Kamera ya AI 3.0 kwenye kamera kuu ya 13MP yenye kipenyo kikubwa cha F/1.8 inaruhusu upigaji picha za kiasili zaidi na zilizo wazi sana usiku na mchana.
Mieko minne ya nyuma inasuluhisha kwa ufanisi tatizo la picha zenye giza ndani ya mazingira ya giza, ambayo inakupatia picha maridadi, angavu na wazi zaidi.

Ugunduzi wa Mandhari wa AI

Ugunduzi 10 tofauti wa mandhari unajumuisha kikamilifu mandhari rahisi na mseto kwa wakati sawia. Pindi mandhari yanapogunduliwa, itatoa uboreshaji linganifu wa AI, ambayo inakuruhusu upige picha hai na bainifu zaidi.

HDR ya AI

HDR ya AI inadhibiti sehemu ya mwangaza isifichuke kupita kiasi, ili kuonyesha sehemu za giza zilizo bainifu na dhahiri zaidi. Kanuni pepe ya kuondoa ukungu inaboresha athari ya jumla ya picha binafsi. Utoaji rangi hauna upungufu na unaonyesha maelezo yote ya kina, ambayo inaifanya picha binafsi ya uso iwe na rangi na udhahiri zaidi.

Athari ya Bokeh ya AI Iliyo Bora na Pana Zaidi

Athari ya Bokeh ya Usuli imesombezwa kikamilifu, ambayo inazipatia picha za uso ulengaji bora kwenye picha nzima pamoja na kusindika maelezo ya kina kwa makini.

Upigaji Picha wa Makro

Picha ya karibu mno inaonyesha maelezo zaidi na inafichua urembo wa mambo madogo yanayokuzunguka.

Kamera ya Picha Binafsi ya AI ya 8MP

Yenye Kamera ya Picha Binafsi ya AI ya 8MP, SPARK 5 daima iko tayari kunasa kumbukumbu zako maridadi.
Kwa kutumia HDR ya Picha ya Uso na mieko miwili ya mbele, picha binafsi angavu na ya kuvutia zaidi ndani ya mandhari ya mwangaza mchache inapigwa kwa urahisi zaidi.
Kanuni pepe ya uso iliyosanifiwa kikamilifu inaokoa muda utakaotumia kujirembesha, ambayo inaleta uzoefu laini na cheshi zaidi wa picha binafsi.

Hali ya Urembo ya AI

Kuweka awali aina tatu za urembo zilizobinafsishwa, kupangusa ngozi na kuangaza kwa busara zote ni sehemu ya Hali ya Urembo ya AI. Marekebisho anuwai kwenye kiolesura cha AI yamefanywa na sasa kinasaidia mwonekano awali wa muda halisi kwa mguso mmoja.

Athari ya Bokeh ya Picha ya Uso 2.0

Usahihi wa kutia ukungu umeboreshwa sana, ambayo inaifanya athari ya bokeh ilenge zaidi kipengee kikuu cha picha ya uso huku inautia ukungu kiasili na kimaizi usuli.

Picha Binafsi Pana

Unapopiga picha binafsi na familia au marafiki, badili pembe ya simu kulingana na maagizo ya skrini, ili kamera iweze kunasa kila mtu kwenye picha na ikupatie picha binafsi pana yenye mwangaza.

Onyesho la Nukta-Ndani la Inchi 6.6

Uzoefu wa mwonekano ulio ang’avu, mpana na tumbukizi kabisa.
Vipimo vya jumla vilivyoboreshwa na radiani ya mjengo wa 3D zinamaanisha inakaa vizuri mkononi. Mwonekano wa juu na uwiano murwa wa skrini wa 90.2% zinachangia kupata uzoefu wa mwonekano kamili ulio mpana na maridadi zaidi.

HiOS 6.0 Mpya

HiOS 6.0 mpya inayotegemea Android Q iko hapa, yenye utekelezaji wa OS na uzoefu wa mwonekano zilizoboreshwa.

Mandhari ya Giza

Mandhari ya Giza mapya hayapunguzi mwasho wa macho kutokana na skrini tu, bali pia inaokoa nishati na kupanua maisha ya betri kwa ufanisi.

Tabo ya Kijamii

Kisanduku cha Kisaidizi cha WhatsApp kilicho bora kabisa chenye vipengele kadhaa vinavyopatikana ili kuongeza ucheshi kwenye mazungumzo na marafiki. Kisanduku cha zana chenye nguvu kinachoweza kuundia Emoji ya DIY, kuhifadhi hali ya sasa ya WhatsaApp, na kuufungua mweko kiotomatiki unapokuwa unapokea simu ya WhatsApp. Vipengele mahiri zaidi vimeongezwa.

Hali ya Urembo ya Gumzo la Video

Inatoa urembo wa AI ndani ya simu ya video ya WhatsApp kwa mguso mmoja tu. Onekana kijana, ang’avu na mwenye bashasha zaidi kwenye gumzo la video.

4G VoLTE

Sasa unaweza kupiga simu kwa ubora wa sauti ulio wazi kabisa unapoongea na familia na marafiki wako wakati simu zote mbili zinatumia shughuli hii.
(*Mhudumu wa mtandao anafaa kusaidia shughuli hii.)

Usanifu

Mipindo bainifu ya uhariri na machaguo murwa ya rangi ya upinde yanaifanya SPARK 5 mpya ivutie kila mtu. Machaguo zaidi kwa mtindo wako wa kipekee.

Nishati Murwa ya 5000mAh

Iambie kwaheri akiba yako ya nishati. Betri yenye nguvu ya 5000mAh na mfumo maizi wa kuokoa nishati zinakidhi mahitaji yako ya kuwa na nishati kila siku kwenye maisha na kazi yako.

ROM ya 32GB + RAM ya 2GB

ROM ya 32GB ROM inatoa nafasi ya kutosha ili kuhifadhi picha unazozipenda na faili muhimu. RAM ya 2GB inafikisha utekelezaji imara na laini kwenye mfumo wetu. Kufanya shughuli anuwai kwa wakati mmoja kumekuwa na urahisi na upesi zaidi.

Kufungua kwa Uso 2.0

Tambua kiotomatiki macho yako yaliyofumbwa, ambayo inaboresha sana usalama na faragha ya simu yako.