Lagos, Julai 10, 2017 — TECNO Mobile, mtengenezaji simu za mkononi anayeongoza na ‘Mbia Rasmi wa Tableti na Simu wa Klabu ya Kandanda ya manchester City’, imezindua simu yake maizi ya toleo la Manchester City la Camon CX.
TECNO Camon CX ndiyo ya hivi sasa zaidi katika msururu wa simu maizi zinazoangazia picha wa TECNO Camon; msururu unaojulikana zaidi kwa maboresho ya hali ya juu ya kamera na bei nafuu zaidi. Toleo la Manchester City la Camon CX lina rangi ya buluu ya klabu ya City na linajumuisha nembo rasmi upande wa nyuma.
Toleo la Manchester City la Camon CX inasalia kuwa ya kweli katika kihisio chapikseli na teknolojia za kusafisha picha za vifaa vya hivi sasa zaidi vya Camon CX/ CX Air.
“Simu hii maizi, kama tu wenzake, TECNO CX/CY Air, ina kamera mbili zeneye teknolojia ya kusafisha picha ya 4 ndani ya 1. Hii inamaanishwa uwezo wa uwiano wa mitambo na usafishaji (SNR) ni mara 1.7 bora zaidi kuliko simu maizi wastani na ina uwezo wa ajabu wa kupiga picha maridadi na za ajabu katika mwangaza mchache.” alisema Stephen Ha, Meneja Mkuu wa TECNO Mobile.
Kila pikseli kwenye kamera za mbele na nyuma za MP 16 zinagundua na kuwasilisha mwangaza kutoka kwenye picha kama mitambo huru ambayo inaunganika ili kuunda picha ya mwisho. Teknolojia hii ya hali ya juu ya kamera inapelekea selfi ambazo ni ng’aavu zaidi kwa asilimia thelathini kuliko selfi za simu maizi wastani.
Vifaa 5000 vya Toleo la Manchester City la Camon CX vitapatikana katika maeneo tisa kote ulimwenguni ikijumisha Naijeria, Kodivaa, Ghana, Mali, Kenya, Tanzania, Dubai, Saudia na Kameruni.
“Ili kusherehekea ushirikiano wetu na Manchester City, tunajivunia kuwapa watumiaji wetu huduma isiyolingana na nyingine kwa kutoa simu maizi mpya ya Toleo la Manchester City la Camon CX.” Stephen aliongeza.
Simu maizi hii ya kipekee ina vipengele vya kipekee kama vile muundo wa chuma wa rangi ya buluu ya klabu ya City, nembo ya Manchester City ya ngozi kwenye upande wa nyuma na nafasi ya hifadhi iliyo boreshwa ya RAM ya GB 4/ ROM ya GB 64, kubwa zaidi kuliko ya Camon CX.
Wateja wa TECNO wanaofungua boksi upya ya simu hii mpya pia watafurahia vifurushi vya zawadi vilivyobinafsishwa ikijumuisha kijiti cha kupiga picha ya selfi, chupa ya maji na spika za bluetooth zote zikiwa na nembo ya klabu ya City.
Toleo la Manchester City la Camon CX litaanza kusafirishwa hadi Naijeria, Kenya na Dubai, na vile vile hadi kwenye masoko mengine teule. Bei halisi itatofautiana katika masoko.