TECNO SPARK na SPARK Plus inaleta vipengele vizuri ambavyo si vya kawaida katika vifaa vya aina hii.
- Flashi Mseto: Flashi Mseto imechanganyisha flashi ya mbele, flashi ya skrini pamoja ili kuleta ung’aavu zaidi na bado kusawazisha rangi za ngozi. Na ina kamera ya mbele ya MP 5 na kamera ya nyuma ya MP 13 na lenzi ya picha ya 5P na kioo cha buluu kinachoimarisha nguvu chujio la kioo kwa 50% na kutoa picha safi zaidi.
- Skrini ya Mwangaza wa Jua: Skrini ya HD ya IPS ya 5.5”. Na ung’aavu wa skrini sasa ina ng’aa zaidi kwa 12.5% kuliko skrini wastani ili kutoa athari safi na ng’aavu zaidi unapotazama picha.
- Miliki Usiku: Ikisawazishwa na apecha ya F/2.0 ya kamera ili kuwezesha picha bora zaidi na ng’aavu zaidi katika mazingira ya mwangaza mchache kama picha za usiku na ndani ya chumba, TECNO SPARK na SPARK Plus inaweka kiwango kipya cha picha kwenye simu maizi.
- Utambuaji Thabiti wa Ung’aavu: Inapogunduliwa kwamba mwangaza wachumba ni mchache, SPARK inatumia “Visidon highlight algorithm” ili kusaidia kuimarisha ung’aavu wa picha na kutoa usawazishaji rangi nyeupe kiotomatiki, na kukuwezesha kuona na kupiga picha zinazokaa halisi.
- Utambuaji Uso: Katika mchakato wa kupiga picha ya uso, utambuaji sahihi wa vipengele vya uso, kuangazia maelezo ya uso, ili ngozi yako ionekane changamfu zaidi.
Stephen Ha, Meneja Mkuu wa TECNO Mobile alisema: “Kama kampnuni ya vifaa vya mkononi iliyobunifu na thabiti kabisa, tuna imani katika kauli yetu ya kuwasaidia watumiaji kupata mengi zaidi na hiyo ndiyo dhana halisi katika bidhaa hizi mpya. Hizi si simu maizi za kawaida wastani zinazopatikana sokoni, hizi ni bidhaa za kisasa na bunifu sana ambazo zinaweza kushindana na bidhaa kadhaa za hali ya juu zinazopatikana leo.”
Kando na vipengele hivyo vya uimarishaji kuhusiana na flashi na kamera, TECNO SPARK na SPARK Plus pia zinatoa vipengele bunifu ikijumuisha: Picha za alama ya kidole zinazokuwezesha kufurahia utumizi kwa mkono mmoja, hali ya kamera ya panorama ya selfi ya pembe pana ya digrii 120 na pita ya uwiano wa mraba wa 1:1 na kufanya kushiriki picha zako bora kwenye Instagram kuwa rahisi ajabu.
Betri ya mAh 3000, athari 8 za kufanya maridadi, OS ya Android 7.0 Nougat ndivyo vipengele vingine muhimu vya TECNO SPARK huku SPARK Plus ikiwa na vipengele vya juu zaidi kama skrini ya HD ya 6.0”, RAM ya GB 2, ROM ya GB 16 na betri ya mAh 3400 mAh.
TECNO SPARK na SPARK Plus itasafirishwa hadi Naijeria katikati mwa mwezi Agosti na bei halisi zitakuwa kulingana na masoko ya nchini.