MANCHESTER CITY INASHEREHEKEA USHIRIKIANO WA KIULIMWENGU WA TECNO MOBILE

Manchester, 30 Novemba – Bidhaa ya hali ya juu ya simu ya mkononi, TECNO Mobile, Manchester City ya Ligi Kuu ya Uingereza, leo wanasherehekea uzinduzi wa ushirikiano wao mpya wa kiulimwengu wa miaka mingi.

 

Manchester, 30 Novemba – Bidhaa ya hali ya juu ya simu ya mkononi, TECNO Mobile, Manchester City ya Ligi Kuu ya Uingereza, leo wanasherehekea uzinduzi wa ushirikiano wao mpya wa kiulimwengu wa miaka mingi.

Kama Mbia Rasmi wa Tableti na Simu za Mkononi wa Klabu cha Kandanda cha Manchester City, TECNO Mobile itashirikiana na Klabu hiki ili kukuza matangazo yake ya uuzaji kote ulimwenguni, ikijumuisha Afrika ambako TECNO tayari inatambuliwa sokoni kama bidhaa inayoongoza ya simu za mkononi.

 

TECNO, sehemu ya Transsion Holdings, ilianzishwa nchini Uchina na katika muongo uliopita imekuza uwepo wake ulimwenguni hadi kwenye masoko 40 yanayoibuka, ambako kuna mashabiki wengi wa klabu ya City na wanaoongezeka kila siku.

Akizungumza katika uzinduzi wa ushirikiano wa kiulimwengu, uliofanyika katika Chuo cha Kandanda cha City, kituo cha hali ya juu cha mafunzo na ukuzaji vijana cha Manchester City, Tom Glick, Afisa Mkuu wa Biashara wa City Football Group, alisema: “Tunafurahia sana kukaribisha TECNO Mobile katika orodha ya wabia wa kiulimwengu wanaoongezeka wa Manchester City. Lengo lake la kiulimwengu likiandamana na jitihada katika kila soko linaonyesha maadili yake na tunatazamia kushirikiana nao ili kuunganisha na mashabiki wa Manchester City kote ulimwenguni.”

Stephen Ha, Meneja Mkuu wa TECNO Mobile, akizungumza katika hafla ya uzinduzi katika Chuo cha Kandanda cha Manchester City aliongezea: “Tunajivunia kushirikiana na klabu yenye mafanikio na maarufu kama Manchester City, na kuendeleza uhusiano wetu mrefu na michezo katika kiwango cha juu. Kuwapa watumiaji wetu huduma zisizolingana na nyingine za vifaa vya mkononi ndicho kipaumbele cha juu zaidi cha TECNO Mobile na tunaona mambo mengine yanayolingana na haya katika Machester City tunapotazama jitihada zao za kuleta mechi nzuri na huduma ya kidijitali kwa mashabiki wao. Tunafuraha kujiunga na timu yao na tuna hamu sana ya kuanzisha ushirikiano huu wetu wa pamoja.”