TECNO, Lagos – Bidhaa inayoongoza ya simu maizi na simu za kawaida, TECNO inaangazia tena mkakati wake wa uuzaji ili kuchukua soko la Mashariki ya kati na Amerika Kusini kufuatia mafanikio katika soko la Afrika. Kiongozi wa Uuzaji na Mahusiano wa TECNO, Attai Oguche, alithibitisha ripoti za kuwa na mgao mkubwa zaidi wa soko katika masoko sita ya Afrika yakiwa ni: Naijeria, Ghana, Kenya, Ethiopia, Tanzania and Kameroon katika Uzinduzi wa Kimataifa wa TECNO katika jengo la Burj Khalifa, Dubai.
“Tunafurahishwa na ripoti ya hivi majuzi inayoiweka TECNO kama bidhaa ya simu nambari moja ya Afrika; ikiwa na mgao wa soko wa wastani wa 25.3% katika masoko yote makuu katika eneo la chini ya jangwa la Sahara. Kwa sasa, Naijeria na Tanzania ndiyo masoko yetu makubwa zaidi” alisema Attai Oguche.
Phantom6
Akizungumza katika uzinduzi wa simu ya sasa zaidi ya Phantom ya TECNO, TECNO Phantom 6, meneja wa uuzaji wa bidhaa kidigitaji wa TECNO Nijeria, Jesse Oguntimehin alizungumzia vipengele muhimu vya simu mpya maizi ya Phantom 6
“Tunajivunia sanakuzindua simu maizi nyembamba zaidi sokoni yenye kamera mbili za nyuma, TECNO Phantom 6 mpya ina wembamba wa 7.05mm katika sehemu iliyonono zaidi,” alisema Jesse Oguntimehin, kiongozi wa uuzaji kidijitali wa TECNO, Naijeria.
Akizungumzia sera zilizoboreshwa za bidhaa za baada ya mauzo kwa watumiaji vifaa vya mkononi wa Naijeria, meneja wa Uuzaji na Uhusiano na Umma wa TECNO, Attai Oguche alisema watumiaji sasa wanaweza kufurahia hakikisho la miezi kumi na tatu (13), kipindi cha ukarabati cha saa 24, siku 15 za kubadilishiwa DAP bila malipo na miezi mitatu ya bima dhibi ya skrini kuvunjika kwenye simu maizi mpya ya Phantom 6 Plus.
“Tunasalia wakweli kwa kauli yetu ya kampuni ya “Experience More” (Pata Mengi Zaidi) katika ubunifu na huduma kwa wateja. Mafanikio ya TECNO katika masoko yanategemea sana kwenye utumizi wa maoni ya watumiaji katika mfumo wetu ili kuwasilisha huduma zilizobinafsishwa kwa watumiahi kote katika masoko.”Attai alisisitiza.
Jumla ya programu 32 tofauti zinaweza kuendeshwa wakati mmoja kwa pamoja kwenye Phantom 6 Plus bila ya kuathiri utendakazi wake. Ikiwa na kumbukumbu ya kuundiwa ndani ya GB 64 na RAM ya GB 4, Phantom 6 Plus inasifiwa na wakaguzi kama mojawapo ya simu maizi bora zaidi sokoni. TECNO Phantom 6 na 6 Plus pia inaanzisha utumizi wa teknolojia ya mapinduzi ya kuchaji kwa haraka ya kituo cha Type-C.
“Kituo cha USB cha Type-C inaruhusu kugeuza plagi, kuchaji na kutuma data kwa haraka kutoka kwa Phantom 6 hadi kwa vifaa vingine,” Jesse Oguntimehin alisema.
Mwaka wa 2015, TECNO Mobile ilipokea tuzo la Taji la Ubora la Kimataifa, kategoria ya dhahabu mjini London na Simu maizi inayomwangazia Mteja zaidi, Maonyesho ya Uchumi wa Vifaa vya Mkononi ya Naijeria (NiMES 2015) nchini Naijeria.
Kama sehemu ya mkakati wake wa kukua katika masoko mapya, TECNO Mobile imeanza kutoa mipango yake ya kuingia katika masoko ya Asia Kusini mashariki na Amerika Kusini kufuatia mafanikio katika kuingia soko la Mashari ya Kati.