TECNO MOBILE YAZINDUA PHANTOM 8 MPYA BARANI MASHARIKI YA KATI

Nyongeza mpya zaidi ya TECNO Phantom inatoa picha halisi, za haraka zaidi, bunifu na maridadi kuweza kupigwa Dubai inatenda kama kituo cha uzinduzi wa kanda cha TECNO, mtengenezaji simu maizi anayeongoza

Dubai, Falme za Kiarabu, Oktoba 23, 2017 – TECNO, bidhaa ya hali ya juu ya simu za mkononi shinya kampuni ya TRANSSION HOLDINGS, imezindua ongezeko lake la hivi sasa zaidi, Phantom 8 katika kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika. Uzinduzi wa kanda ulifanyika katika Hoteli ya Jumeirah Beach, Dubai na kuhudhuriwa na wageni 200.

Phantom 8 iliyozinduliwa upya inayoendeshwa na Android ina kamera ya ajabu, muundo wa kuvutia na huduma ya kasi. Kulingana na Google’s Consumer Barometer, nchini UAE na KSA, 73% na 70% ya watumiaji simu maizi wanatumia simu zao kupiga picha na kurekodi video. Phantom 8 inashughulikia hitaji hili la ndani kwa kamera zake mbili za hali ya juu, ina nguvu ya kufanikisha uvutaji karibu wa mara 10 na pia kuleta fokasi tena kiotomatiki.

“Kanda ya MEA ni thabiti na inafurahia ubunifu maizi pamoja na muundo maridadi unaopendeza. Phantom 8 inaangazia mahitaji ya kanda hii na ina nguvu zaidi kuliko hapo awali katika kazi na ubora wa picha,” alisema Arif Chowdhury, Naibu Rais wa TRANSSION HOLDINGS.

“Tunafurahia kuendelea na safari yenye mafanikio barani Mashari ya kati na Afrika ili kuleta huduma iliyoimarika ya vifaa vya mkononi kwa wale walio katika kanda hii,” alihitimisha.

TECNO Mobile ndiyo bidhaa ya hali ya juu ya simu inayolenga kuunda mfumo ekolojia wa burudani uliobinafsishwa kulingana na mahitaji na tabia za watumiaji wachanga kote kati masoko kwenye jukwaa la Android. Ubinafsishaji huu unatofautiana kwa kila soko na kila watumiaji lengwa.

Phantom 8 ya TECNO Mobile inakuja na kamera ya mbele ya megapikseli 20 pamoja na flashi mbili mazi za selfi. Zaidi ya hayo, flashi mbili za mbele za pete zinahakikisha unaweza kupiga picha hata katika mazingira yenye mwangaza mchache. Unapata dakika 150 za kuzungumza baada ya kuchaji betri kwa dakika 10 pekee, bei yake ni 1399 AED.
Muundo wa mtindo wa Almasi wa Phantom 8 unakuja na mwangaza wa 3D Lighting, mwili mmoja wa chuma na kifuniko cha betri kilikunjwa pamoja na skrini cha 2.5 D. Pia ina RAM ya GB 6 na vile vile CPU yenye kasi kupindukia ya 2.6 GHz inayoruhusu 4G+ na kasi ya kupakua ya hadi 300Mbps.

Phantom 8 mpya inatangamana na Kadi ya Maikro SIM au Nano SIM na kuruhusu hadi kadi ya TF (Trans Flash) ya TB 2 (Terabaiti), na ina moduli 4, bendi 20 na inakubali zaidi ya nchi na kanda 200.