TECNO PHANTOM 6 NA 6 PLUS: UZINDUZI WA KIMATIAFA WA SIMU MAIZI ZA KIMATAIFA

Tukio la ajabu lilihudhuriwa na vyombo 80 vya habari vya nchini na vya kimataifa kama vile Al Khaleej, Emirates news, Gulf News, Deutsche Presse-Agentur DPA, Xinhua News Agency n.k.

Tukio la ajabu lilihudhuriwa na vyombo 80 vya habari vya nchini na vya kimataifa kama vile Al Khaleej, Emirates news, Gulf News, Deutsche Presse-Agentur DPA, Xinhua News Agency n.k. Tukio hili pia lilishuhudiwa na wageni wengi mashuhuri kama vile Kimura Makoto, Meneja Mkuu wa SONY, Jeremy Doutte, Afisa Mkuu Mtendaji wa Jumia, Arthur Wang, Mkurugenzi Mkuu wa Mauzo ya Kimataifa wa MediaTek; Martin Kariithi, Meneja wa Mashirikiano ya Android wa Google (Afrika Magharibi) na bila kusahau watu maarufu wa Naijeria, VJ Adams na Mercy Aigbe Gentry, na vile vile watu wengine maarufu.
PhantomPhantom

Katika muongo uliopita, TECNO mobile imewika katika soko la vifaa vya mkononi la Afrika na kuwa bidhaa maarufu zaidi katika eneo hili. Mara kwa mara ikitengeneza vifaa vya hali ya juu vya simu maizi, ongezeko hili la hivi sasa zaidi kwenye msururu wa TECNO Phantom – Phantom 6 na Phantom 6 Plus pia zinajumuishwa hapa. Vifaa hivi vipya vinajivunia maboresho kadhaa ya hali ya juu ikilinganishwa na vifaa vilivyotanguliua, Phantom Z na Phantom 5 iliyozinduliwa mwaka wa 2014 na 2015 mtawalia.

Maboresho ya ajabu: Lenzi mbili za nyuma nyembamba zaidi na phantom yenye kamera ya Sony ya MP 21
phantom

Ikiwa na muundo mwembamba zaidi wa 6.15mm, Phantom 6 ina taji la kuwa simu maizi nyembamba zaidi yenye lenzi mbili za nyuma, na kuibwaga iPhone 7 mpya (7.3mm) na Huawei P9 mpya (9mm) ambazo hapo awali zilisifiwa kuwa simu maizi nyembamba zaidi.
phantom

Ikiwa na kamera mbili za nyuma za MP 13 na MP 5 za fokasi otomatiki zenye flashi ya LED, Phantom 6 pia ina nafasi kubwa ya hifadhi kwa utendakazi bora zaidi; ikiwa na RAM ya GB 3 na ROM ya GB 32 inayoweza kunenepeshwa hadi GB 128, na kuendeshwa na visindikaji vya MediaTek Octa-core vya kasi ya 2.0GHz.

Upande mwingine, TECNO Phantom 6 Plus mpya ina skrini nzuri ya kugusa ya IPS ya inchi 6.0 na usalama wa kwanza wa TECNO wa ngazi tatu kwenye simu maizi (alama ya kidole, kifaa cha kuskani jicho na kiua virusi cha TrustLook). Kifaa hiki pia kinajivunia kisindikaji chenye kasi ya juu zaidi ulimwenguni cha Mediatek Helio ×20 Deca core pamoja na RAM ya DDR3 ya GB 4 na ROM ya GB 64, inayoweza kunenepeshwa hadi GB 256.

 Vifaa hivi viwili vya Phantom vina kituo cha USB cha Type-C chenye uwezo wa kuchaji kwa haraka kupindukia.
Bidhaa Na. 1 Afrika ya simu maizi inasherehekea miaka 10

Kiongozi bila upinzani wa simu maizi barani Afrika, TECNO ilisherehekea maadhimisho yako ya mwaka wa kumo katika uzinduzi wa Phantom 6 mpya mjini Dubai. Kampuni hii ya Uchina iliyo katika mataifa mengi illingia katika ulingo wa vifaa vya mkononi wa Afrika yenye hamu kuu ya kuwa kiongozi wa soko hili; ikileta upya teknolojia za aina yake na kwa utaratibu kuchukua mgao wa soko wa bidhaa maarufu barani Ulaya kama vile Nokia, Motorola, Sagem n.k. Tukitazama miaka kumi nyuma, ni salama kusema kwamba TECNO imeweka kigezo thabiti kiasi kwamba chombo kipya kuingia sokoni atakuwa na wakati mgumu kukua.Phantom6 
 ptm6