January 2019, Dar es Salaam, Tanzania – TECNO Tanzania katika kampeni yao ya kuisaidia jamii iitwayo Kuwa Shujaa Wangu kwa kutoa michango katika kituo cha kulelea watoto cha Chanika. Zoezi hili ni muendelezo wa lile la awali lililofanyika mwaka 2018, Novemba. kampuni iliratibu uchangishaji wa misaada kutoka kwa wasamaria wema kupitia mitandao ya kijamii na maduka yote ya Smart Hub.
TECNO iliweza kuchangia Tsh millioni 5 pamoja na misaada mbalimbali kama; mchele, unga, mafuta, sabuni, maji, juisi, pamoja na misaada mingine muhimu ya kijamii. Kampuni inawashukuru wote waliojitolea na wanaoendelea kujitolea kuwasaidia watoto hawa. Tunawakaribisha wasamaria wema wote kuunga mkono kampeni hii ya ukombozi wa jamii ya Tanzania.