TECNO Tanzania yazindua rasmi kampeni yake mpya ya kuisaidia jamii iitwayo, Kuwa Shujaa Wangu.

November 2018, Dar es Salaam, Tanzania – TECNO Tanzania ilizindua rasmi kampeni yake mpya iitwayo Kuwa Shujaa Wangu kama jukumu la kujitolea kuisaidia jamii (Corporate Social Responsibility). Kampeni hii ina lengo ya kuwashika mkono watu waliokatika mazingira magumu. Zoezi lilianzia kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Chanika Children Center kinachosimamiwa na Pannasekara Rev ILukpitiye, kiongozi wa dhehebu la Buddha Tanzania.

TECNO iliweza kupeleka misaada mbalimbali kama vile; mchele, unga, maji, sabuni, juisi, mipira, biskuti n.k. Zoezi hili liliratibiwa pia katika mitandao ya kijamii na maduka ya TECNO Smart Hub ilikuwezesha ukusanyaji misaada kwa ajili ya kituo hichi. Pichani kutoka kushoto waliosimama ni, Pannasekara Rev ILukpitiye (Mkuu wa kituo cha Chanika), msaidizi wake, wasamaria wema kutoka Sri Lank. Chini kutoka kushoto ni, Benson Mambosho (Msimamizi wa idara ya kidijitali TECNO), William Motta (Meneja msaidizi masoko TECNO), Frank Luo (Meneja wa Masoko TECNO) na Eric Mkomoya (Msimamizi wa mahusiano ya umma TECNO).