UZUnDUZI WA SIMU MAIZI YA CAMON CX YA TECNO MOBILE UNATAZAMIWA KUTIKISA SOKO LA AFRIKA

Nairobi, Kenya, Machi 23, 2017 -Bidhaa ya hali ya juu ya simu ya mkononi, TECNO Mobile, leo imezindua simu yake mpya zaidi kuzinmduliwa katika soko la Afrika katika tukio jijini kuu la Kenya, Camon CX.

Nairobi, Kenya, Machi 23, 2017 -Bidhaa ya hali ya juu ya simu ya mkononi, TECNO Mobile, leo imezindua simu yake mpya zaidi katika soko la Afrika katika tukio jijini kuu la Kenya, Camon CX.
Imeundwa haswa kwa ajili ya watumiaji wachanga na huru wa simu maizi, simu ya hivi sasa zaidi itakuwa “Kamera ya Selfi” ya kizazi cha soko hili.
Camon CX itapatikana katika nchi 41 kote barani Afrika, Mashariki ya Kati na Amerika Kusini, na kuwawezesha watumiaji kupiga selfi ng’aavu zaidi, safi zaidi na haraka zaidi kuliko hapo awali.
Tangu msururu wa Camon kuletwa upya mwaka wa 2015, zaidi ya simu milioni 5 zimeuzwa kote ilimwenguni, na kuwasaidia watumiaji kufurahia teknolojia ya selfi ya ubora wa juu kwa kugusa tu kitufe.Kuchukua nafasi yake kama muuzaji anayeongoza wa simu maizi katika masoko ya Afrika kama vile Nijeria, Tanzania, Misri, Kenya na Kameruni, TECNO Mobile inatumia teknolojia ya kisasa zaidi ya kupiga picha kwenye Camon CX.

Simu hii maizi inatumia kihisio maizi cha picha chenye mga pikseli 16 katika kamera ya mbele, yenye teknolojia ya kipekee ya ‘4 ndani ya 1’.
Kila kihisio cha pikseli kinagundua mwangaza na kupiga picha binafsi na kubadilisha taarifa hiyo kuwa mitambo kabla ya kutengeneza picha ya mwisho, na kupelekea selfi ambazo ni ng’aavu zaidi kwa asilimia 30, na kurekodi nyakati maalam kwa njia bora zaidi.
Teknolojia ya ‘4 ndani ya 1’ pia inashirikiana na teknolojia fanisi ya kusafisha picha, na kupata uwiano wa kati ya mtambo na usafi (SNR) mara 1.7 vyema zaidi, ikiwa na teknolojia mpya zaidi ya Usafishaji Maizi ili kutoa picha safi kiajabu hata kwenye mwangaza mchache. Kipengele cha kamera mbili za mbele kinafanya hata mengi zaidi, na kuwezesha watumiaji wa Camon CX kupiga selfi zenye ubora wa ajabu katika mazingira yenye giza ambako hapa awali mwangaza wa kuwekwa unegharibu picha.
Simu hii maizi pia inajumuisha vipengele kama vile flashi iliyobinafsishwa ya pete, kuchaji kwa haraka upesi na skrini ya inchi 5.5 ya FHD (Full High Definition), zote zikiwezesha utumizi kwa urahisi wakati wowote na pia picha za ubora wa juu zaidi.
TECNO, sehemu ya Transsion Holdings, imekuwa na zaidi ya asilimia 25 ya mgao wa soko katika nchi cha Afrika chini ya Jangwa la Sahara tangu mwaka wa 2014. Mauzo katika soko la Afrika yalifikia vifaa milioni 25 mwaka wa 2015, ikijumuisha simu maizi milioni 9. Kote ulimwenguni, iliuza vifaa milioni 60 mwaka uliopita huku mauzo ya simu maizi zilizotengenezwa na kampuni hii yakiongezeka kwa asilimia 40.

Akizungumza katika uzinduzi wa kiulimwengu wa simu maizi ya Camon, Stephen Ha, Meneja Mkuu wa Tecno Mobile, alisema: “Tunafuraha sana kuzindua Camon CX, kama simu yetu maizi mpya zaidi. Jambo la selfi kwa miaka ya hivi majuzi limekithiri katika utumizi wa simu maizi, na ubora wa picha ni muhimu, si tu kwa watumiaji wachanga, lakini kwa demografia pana zaidi za umri. Tumefanya juhudi katika kutumia teknolojia ya hivi sasa zaidi ili kuwapa watumiaji huduma bora zaidi ya vifaa vya mkononi, jambo ambalo ndilo kipaumbele cha TECNO Mobile.”

Beehong Hong, Afisa Mkuu wa Uuzaji wa Transsion, pia alitoa maoni: “Uzinduzi wa Camon CX ndio mfamo wa hivi sasa zaidi wa maeneo ambapo TECNO Mobile inatoa bidhaa za ubora kwa bei nafuu kote katika masoko tofauti. Kifaa hiki haswa kinatupa furaha tunapoingia katika teknolojia mpya, tunawasilisha ubora wa juu zaidi wa picha huku tukitoa kifaa ambacho ni rahisi kutumia. Tunajitahidi kudumisha nafasi ya TECNO kama muuzaji maarufu zaidi wa simu maizi katika soko la Afrika kwa kutumia teknolojia mpya kama ambavyo tumefanya hapa.”